sw_jer_text_reg/31/33.txt

1 line
494 B
Plaintext

\v 33 Lakini hili ni agano nitakaloanzisha na nyumba ya Israeli baada ya siku hizi—hili ni tangazo la Yahwe: Nitaiweka sheria yangu ndani yao na nitaiandika juu ya mioyo yao, kwa maana nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. \v 34 Kisha kila mtu hatamfundisha jirani yake, wala mtu hatamfundisha ndugu yake akisema, 'Mjue Yahwe!' Kwa maana wao wote, kuanzia mdogo wao hata mkubwa, watanijua—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawasamehe uovu wao na sitazikumbuka tena dhambi zao."'