sw_jer_text_reg/25/27.txt

1 line
541 B
Plaintext

\v 27 Bwana akaniambia, "Basi, uwaambie, 'Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi kunywa na kulewa, kisha tapika, uanguke, wala usisimame mbele ya upanga nitakaoutuma kati yenu.' \v 28 Kisha itatokea kwamba ikiwa wanakataa kuchukua kikombe mkononi mwako ili kunywa, utawaambia, 'Bwana wa majeshi asema hii lazima mnywe. \v 29 Kwa maana, tazama, nitaleta janga juu ya mji ulioitwa kwa jina langu, je ninyi mtaachiliwa msiadhibiwe? Hutakuwa huru, kwa maana nitaita upanga juu ya wenyeji wote wa nchi! - ndilo tamko la Bwana wa majeshi.'