sw_jer_text_reg/48/01.txt

1 line
362 B
Plaintext

\v 1 Juu ya Moabu, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Ole kwa Nebo, kwani umekuwa ukiwa. Kiriathaimu umetekwa na kuaibishwa. Ngome zake zimeangushwa na kuaibishwa. \v 2 Heshima ya Moabu haipo tena. Adui zake katika Heshboni walipanga njama za kumwangamiza. Walisema, 'Njoni tumwangamize kama taifa. Madmena pia itaangamizwa - upanga utakutangulia.'