sw_jer_text_reg/29/12.txt

1 line
423 B
Plaintext

\v 12 Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza. \v 13 Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote. \v 14 Kisha nitapatikana kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawarudisha watu wenu waliofungwa; nitawakusanya kutoka mataifa yote na sehemu zote ambako nimewatawanya—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawarudisha kutoka sehemu ambako niliwasababisha kuwa mateka.