sw_jer_text_reg/52/01.txt

1 line
425 B
Plaintext

\v 1 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Jina la mamaye lilikuwa Hamutali; alikuwa binti Yeremia wa Libna. \v 2 Akafanya maovu machoni pa Yahwe; akafanya kila alichokifanya Yehoyakimu. \v 3 Kwa hasira ya Yahwe, matukio haya yote yalitukia Yerusalemu na Yuda, hata alipowatoa mbele yake mwenyewe. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.