sw_jer_text_reg/50/11.txt

1 line
472 B
Plaintext

\v 11 Mnafurahi, mnasherehekea kuteka urithi wangu; mnarukaruka kama ndama anayekanyaga katika malisho yake; mnalia kama farasi mwenye nguvu. \v 12 Hivyo mama yenu ataaibika sana; aliyewazaa atafadhaika. Tazama, atakuwa wa mwisho katika mataifa, atakuwa kama nyika, nchi kame, na jangwa. \v 13 Kwa sababu ya hasira ya Yahwe, Babeli haitakaliwa, lakini itakuwa ukiwa mtupu. Kila apitaye kando ataogopa kwa sababu ya Babeli na ataguna kwa sauti kwa sababu ya majeraha yake.