sw_jer_text_reg/43/08.txt

1 line
521 B
Plaintext

\v 8 Basi neno la BWANA lilikuja kwa Yeremia huko Tahpanhesi na kusema, \v 9 "Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwa bahadhi ya macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi. \v 10 Kisha ukaseme nao, "BWANA wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Ona, nimekaribia kutuma wajumbe kumchukua Nebukadreza mfalme wa Babeli kama mtumwa wangu. Nitaweka kiti cha enzi yake juu ya mawe haya ambayo wewe, Yeremia, umeyazika. Nebukadreza ataweka banda lake juu yao.