sw_jer_text_reg/35/08.txt

1 line
562 B
Plaintext

\v 8 Tumeitii sauti ya Yonadabu mwana wa Rekabu, babu yetu, katika yote aliyotuamuru, kutokunywa divai maisha yetu yote, sisi, wake zetu, wana wetu, na binti zetu. \v 9 Hatutajenga nyumba kwa ajili ya kuishi ndani, na hatutakuwa na shamba la mizabu, konde, wala mbegu ya kumiliki sisi. \v 10 Tumeishi katika hema na tumetii na kufanya yote aliyotuamuru Yonadabu babu yetu. \v 11 Lakini Nebukadreza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi, tulisema, 'Njoo, lazima twende Yerusalemu ili tupone na mkono wa Wakaldayo na majeshi ya Waaramu. 'Kwa hiyo tunaishi Yerusalemu."