sw_jer_text_reg/32/33.txt

1 line
532 B
Plaintext

\v 33 Wamenigeuzia migongo yao badala ya nyuso zao, ingawa niliwafundisha kwa furaha. Nilijitahidi kuwafundisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyenisikiliza ili kupokea marekebisho. \v 34 Walisimamisha sanamu zao za ajabu katika nyumba inayoitwa kwa jina langu, ili kunitia unajisi. \v 35 Wakazijenga sehemu za juu katika Bonde la Beni Hinomu ili kuwatia katika moto wana wao na binti zao kwa ajili ya Moleki. Mimi sikuwaagiza. Sikuweka akilini mwangu kamwe kwamba watafanya mambo maovu na kwa hiyo kuwasabisha Yuda watende dhambi.