sw_jer_text_reg/22/01.txt

1 line
506 B
Plaintext

\v 1 Bwana asema hivi, "Nenda kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda, utangaze neno hili huko. \v 2 Ukaseme, 'Ewe Mfalme wa Yuda, wewe aliyeketi kiti cha Daudi, usikilize neno la Bwana. Nisikilizeni, enyi watumishi wake, na ninyi, watu wake mnaokuja kwa malango haya. \v 3 Bwana asema hivi, "Fanya haki na uadilifu, na mtu yeyote ambaye ameibiwa-muokoeni kutoka mkononi mwa mshindani. Usimtendee mabaya mgeni yeyote katika nchi yako, au yatima au mjane. Usifanye vurugu au kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa.