sw_jer_text_reg/15/19.txt

1 line
560 B
Plaintext

\v 19 Kwa hiyo Bwana asema hivi, "Yeremia, Ikiwa utatubu, nitakurejesha, nawe utasimama mbele yangu na kunitumikia. Kwa maana ukitenganisha mambo ya kipumbavu kwa vitu vya thamani, utakuwa kama kinywa changu. Watu watakuja kwako, lakini wewe mwenyewe usirudi kwao. \v 20 Nitakufanya kama ukuta wa shaba usioweza kuingilika kwa watu hawa, nao watapigana vita dhidi yako. Lakini hawatakushinda, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe ili kuokoa na kukuponya-hili ndilo tamko la Bwana- \v 21 kwa maana nitakuokoa mikononi mwa waovu na kukukomboa katika mkono wa mshindani."