sw_jer_text_reg/44/15.txt

1 line
656 B
Plaintext

\v 15 Kisha watu wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakichoma ubani kwa miungu mingine, na wanawake wote waliokuwa katika kusanyiko kuu, na watu wote ambao walikuwa wakiishi kwenye nchi ya Misri katika Pathrosi walimjibu Yeremia. \v 16 Walisema, "Kuhusu neno ambalo mmetuambia sisi kwa jina la Yahwe: Hatutakusikiliza. \v 17 Kwa hakika tutafanya mambo yote ambayo tulisema tungefanya: kuchoma ubani kwa malkia wa Mbingu na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake kama sisi, mababu zetu, wafalme wetu, na viongozi wetu walivyofanya kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Kisha tutajazwa pamoja na chakula na tutafanikiwa, pasipo kupata maafa yoyote.