sw_jer_text_reg/31/27.txt

1 line
353 B
Plaintext

\v 27 Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapoipanda nyumba ya Israeli na Yuda pamoja na wazawa wa wanadamu na wanyama. \v 28 Zamani, niliwaweka katika uangalizi ili kuwang'oa na kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu, na kuwaletea madhara. Lakini katika siku zijazo, nitawaangalia, ili niwajenge na kuwapanda—hili ni tangazo la Yahwe.