sw_jer_text_reg/27/16.txt

1 line
522 B
Plaintext

\v 16 Nilitangaza hili kwa makuhani na watu wote na kusema, "Yahwe anasema hivi: Msisikilize maneno ya manabii wanaotabiri kwenu na kusema, 'Angalia! Vyombo vya nyumba ya Yahwe vinarudishwa kutoka Babeli sasa hivi!' Wanatabiri uongo kwenu. \v 17 Msiwasikilize. Mtamtumikia mfalme wa Babeli na mtaishi. Kwa nini mji huu uangamizwe? \v 18 Kama ni manabii, na kama neno la Mungu limekuja kwao kweli, basi wamwombe Yahwe wa majeshi asivipeleke Babeli vyombo vilivyosalia katika nyumba, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu.