sw_jer_text_reg/10/14.txt

1 line
396 B
Plaintext

\v 14 Kila mtu amekuwa mjinga, hawana maarifa. Kila mfua chuma ameaibishwa kwa sanamu zake. Maana sanamu yake ya kuyeyushwa ni uongo; hakuna pumzi ndani yake. \v 15 Ni ubatili tu, ni kazi ya udanganyifu; zitapotea wakati wa hukumu. \v 16 Lakini Mungu ni fungu la Yakobo, si kama hawa, kwa kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; BWANA wa majeshi ndiye jina lake.