sw_jer_text_reg/39/01.txt

1 line
507 B
Plaintext

\c 39 \v 1 Katika mwaka wa tisa na mwezi wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalemu na kuizingira. \v 2 Katika mwaka wa kumi na moja na mwezi wa nne wa Sedekia, siku ya tisa ya mwezi, mji uliharibiwa. \v 3 Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli walikuja na kukaa kwenye lango la katikati: Nergali Sharezeri, Samgari Nebo, na Sarsechimu, afisa muhimu. Nergal- Shareza alikuwa afisa mkuu na wote waliobaki maafisa wa mfalme wa Babeli.