sw_jer_text_reg/50/03.txt

1 line
471 B
Plaintext

\v 3 Taifa kutoka kaskazini litainuka kinyume chake, ili kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja, awe mtu au mnyama, atakayeishi ndani yake. Wataondoka. \v 4 Katika siku hizo na wakati huo--hili ni tamko ya Yahwe--watu wa Israeli na watu wa Yuda watakusanyika ili kwenda kwa kulia na kumtafuta Yahwe Mungu wao. \v 5 Watauliza njia ya kwenda Sayuni nao watakwenda huko, wakisema, tutakwenda wenyewe ili kuungana na Yahwe katika agano la milele ambalo halitasahaulika."