sw_jer_text_reg/48/30.txt

1 line
484 B
Plaintext

\v 30 Hili ni tamko la Yahwe--Mimi mwenyewe najua maneno yake ya ukaidi, yasiyosaidia chochote, kama matendo yake. \v 31 Hivyo nitavumisha maombolezo kwa ajili ya Moabu, na nitapiga kelele katika uzuni kwa ajili ya Moabu. Nitaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir Hereshi. \v 32 Nitalia zaidi kwa ajili yenu kuliko nilivyofanya kwa Yazeri, mzabibu wa Sibma! Matawi yako yalipita katika Bahari ya Chumvi na kufika hata Yazeri. Mwaribu ameshambulia matunda yenu ya kiangazi na mzabibu wenu.