sw_jer_text_reg/47/03.txt

1 line
420 B
Plaintext

\v 3 Kwa sauti ya vishindo vya kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa ngurumo za magari yao ya kivita na kelele za magurudumu yake, wababa hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wa mikono yao. \v 4 Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia huko Tire na Sidoni anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahwe anawaangamiza Wafilisiti, hao waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.