sw_jer_text_reg/51/57.txt

1 line
481 B
Plaintext

\v 57 Maana nitawafanya wana wafalme wake, wenye hekima wake, watawala wake, na wakuu wake, na maaskari wake kulewa, nao watalala usingizi kwa usingizi usioisha na bila kuamka--hili ni tamko la mfalme: Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. \v 58 Yahwe wa majeshi asema hivi: Ukuta mnene wa Babeli utabomolewa kabisa, na malango yake marefu yataunguzwa. Kisha watu wanaokuja kumsaidia watafanya kazi isiyofaa; kila mataifa wanachojaribu kikifanya kwa ajili yake kitateketezwa kwa moto."