sw_jer_text_reg/51/25.txt

1 line
393 B
Plaintext

\v 25 Tazama, mimi ni kinyume chako, ewe mlima, wewe unayewaharibu watu wengine--hili ni tamko la Yahwe--kuiharibu dunia yote. Nitakupiga na mikono yangu na kuvingirisha chini kutoka ukingo wa kilima. Kisha nitakufanya mlima ulioteketezwa kabisa kwa moto. \v 26 Hivyo hawatachukua kwako jiwe lolote ili kujengea pembe ya nyumba au msingi; kwani utakuwa ukiwa wa milele--hili ni tamko la Yahwe.