sw_jer_text_reg/50/35.txt

1 line
393 B
Plaintext

\v 35 Upanga u juu ya Wakalidayo--asema Yahwe--na juu ya wakaao Babeli, viongozi wake, na wenye hekima wake. \v 36 Upanga unakuja juu ya waganga, ili wajione kuwa wajinga. Upanga utakuwa juu ya askari wake, hivyo watajaa hofu. \v 37 Upanga waja juu ya farasi wake, vibandawazi vyao na na watu wote waliomo Babeli, hivyo watakuwa kama wanawake. Upanga utakuwa juu ya ghala zake, nazo zitatekwa.