sw_jer_text_reg/48/15.txt

1 line
400 B
Plaintext

\v 15 Moabu itaangamizwa na miji yake kushambuliwa. Kwa maana vijana wake wazuri wameshuka katika eneo la machinjo. Hili ni tamko la mfalme! Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. \v 16 Maangazizo ya Moabu yanakaribia; maafa yanaharakisha upesi. \v 17 Ninyi nyote mlio karibu na Moabu, ombolezeni; nanyi wote mjuao fahari yake, pigeni kelele hivi, 'Ole, fimbo yenye nguvu, fimbo yenye heshima, imevunjwa.'