sw_jer_text_reg/47/01.txt

1 line
408 B
Plaintext

\c 47 \v 1 Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabii juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza. \v 2 "Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mmoja atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.