sw_jer_text_reg/46/15.txt

1 line
449 B
Plaintext

\v 15 Kwa nini Apis mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahwe amemwangusha chini. \v 16 Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anamwangukia yule anayefuata nyuma yake. Wanasema, "Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuwe mbali na upanga wa mwangamizi." \v 17 Walitangaza pale, "Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, aliyeiacha fursa yake ipotelee mbali."