sw_jer_text_reg/46/01.txt

1 line
568 B
Plaintext

\c 46 \v 1 Hili ni neno la Yahwe lililomjia Yeremia nabii kuhusu mataifa. \v 2 Juu ya Misri; "Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda: \v 3 Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge mbele vitani. \v 4 Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.