sw_jer_text_reg/42/04.txt

1 line
498 B
Plaintext

\v 4 Basi Yeremia nabii alisema nao, "Nimewasikia, Tazama, Nitaomba kwa Yahwe Mungu wenu kama mlivyoomba. Vyovyote Yahwe atavyonijibu, Nitawambia. Sitawaficha chochote ninyi." \v 5 Walisema na Yeremia, "Na Yahwe awe shahidi mkweli na mwaminifu dhidi yenu, kama hatutafanya kila kitu ambacho Yahwe Mungu wenu atwambia kufanya. \v 6 Hata kama ni vizuri au vibaya, tutatii sauti ya Yahwe Mungu wetu, ambaye tunawatuma ninyi, ili kwamba iwe vizuri pamoja nasi wakati tunatii sauti ya Yahwe Mungu wetu."