sw_jer_text_reg/42/01.txt

1 line
437 B
Plaintext

\c 42 \v 1 Kisha maamiri wote wa jeshi na Yohanani mwana wa Karea, Jezania mwana wa Hoshaia, na watu wote kutoka mdogo hadi mkubwa walimkaribia Yeremia nabii. \v 2 Walisema naye, "Acha maombi yetu yaje mbele yako. Omba kwa ajili yetu kwa Yahwe Mungu wako kwa ajili ya watu hawa ambao wanabaki kwani tuko wachache katika idadi, kama unavyoona. \v 3 Muulize Yahwe Mungu wako atuambie sisi njia itupasayo kwenda na yapi yatupasayo kutenda."