sw_jer_text_reg/40/07.txt

1 line
563 B
Plaintext

\v 7 Sasa baadhi ya maamiri wa wanajeshi wa Yuda ambao walikuwa bado katika uwanja--wao na watu wao--walisikia kuwa mfalme wa Babeli alimfanya Gedalia mwana wa Ahikam, liwali juu ya nchi. Pia walisikia kuwa amemweka kusimamia wanaume, wanawake, na watoto ambao walikuwa watu maskini katika nchi, wale ambao hawakuwa wamechukuliwa mateka Babeli. \v 8 Basi walienda kwa Gedalia huko Mizpa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana Nethania; Yohanani na Yonathani, wana wa Kareaa; Seraya mwana wa Tanhumethi; wana wa Efai Netofa; na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.