sw_jer_text_reg/40/03.txt

1 line
503 B
Plaintext

\v 3 Basi Yahwe alilileta. Alifanya kama alivyoamrisha, kwani ninyi watu mmefanya dhambi dhidi yake na hamkutii sauti yake. Hii ni sababu ya jambo hili limetokea kwenu. Lakini sasa tazama! \v 4 Nimekuacha huru leo toka kwenye minyororo iliyokuwa kwenye mikono yako. Kama ni vizuri katika macho yako kuja nami Babeli, njoo, na nitakujali. Lakini kama si vizuri katika macho yako kuja pamoja nami, basi usifanye hivyo. Tazama nchi yote mbele yako. Nenda ambapo ni pazuri na sawa katika macho yako kwenda."