sw_jer_text_reg/34/12.txt

1 line
492 B
Plaintext

\v 12 Kwa hiyo neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema, \v 13 "Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Mimi mwenyewe nilifanya agano na babu zenu katika siku ambayo niliwatoa nje ya nchi ya Misiri, nje ya nyumba ya utumwa. Hapo ndipo niliposema, \v 14 Katika mwisho wa mwaka wa saba, kila mtu lazima amwachie ndugu yake, Mwebrania mwenzake aliyejiuza mwenyewe kwako ili kukutumikia kwa miaka sita. Mwagize aende kwa uhuru." Lakini babu zenu hawakunisikiliza wala kutega masikio yao kwangu.