sw_jer_text_reg/30/18.txt

1 line
378 B
Plaintext

\v 18 Yahwe anasema hivi, "Ona, niko karibu kuwarudisha mateka wa hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu, na jumba litakuwepo tena kama ilivyokuwa kawaida. \v 19 Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya ya shangwe itasikika kutoka kwao, kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza; nitawaheshimu ili kwamba wasifanywe wanyonge.