sw_jer_text_reg/25/12.txt

1 line
470 B
Plaintext

\v 12 Kisha miaka sabini itakapokamilika, nitamuadhibu mfalme wa Babeli na taifa hilo, nchi ya Wakaldayo-hili ndilo tamko la Bwana-kwa uovu wao na kuifanya kuwa ukiwa milele. \v 13 Nami nitaleta juu ya nchi hiyo maneno yote niliyosema, na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hiki ambacho Yeremia ametabiri juu ya mataifa yote. \v 14 Kwa maana pia mataifa mengi na wafalme wakuu watapata watumwa kutoka mataifa haya. Nitawalipa kwa matendo yao na kazi za mikono yao.'"