sw_jer_text_reg/20/05.txt

1 line
399 B
Plaintext

\v 5 Nitampa mali zote za jiji hili na utajiri wake wote, vitu vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Nitaweka vitu hivi mikononi mwa adui zako, nao watawakamata. Nao watawachukua na kuwaleta Babeli. \v 6 Lakini wewe Pashuri, na wenyeji wote wa nyumba yako watakwenda mateka. Utakwenda Babeli na kufa huko. Wewe na wapendwa wako wote ambao uliwatabiria maneno ya uongo mtazikwa huko.'"