sw_jer_text_reg/13/08.txt

1 line
562 B
Plaintext

\v 8 Ndipo neno la Bwana likanijia tena, kusema, \v 9 "Bwana asema hivi, Nitakiangamiza kiburi cha Yuda na Yerusalemu. \v 10 Watu hawa waovu wanaokataa kusikia neno langu, ambao huenda katika ugumu wa mioyo yao, ambao hufuata miungu mingine ili kuabudu na kuinama-watakuwa kama hii nguo isiyofaa kwa lolote. \v 11 Kwa maana kama vile vazi lililofungwa kwenye viuno vya mtu, ndivyo nimefainya nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda zimefungwa kwangu- hili ndilo tamko la Bwana-wawe watu wangu, ili kunifanya jina, sifa, na heshima. Lakini hawakunisikiliza.