sw_jer_text_reg/12/10.txt

1 line
303 B
Plaintext

\v 10 Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu. Wameipoteza sehemu yangu yote ya ardhi; Waligeuza sehemu yangu nzuri kuwa jangwa, ukiwa. \v 11 Wamemfanya kuwa ukiwa. Ninaomboleza kwa ajili yake; yeye ni ukiwa. Nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa maana hakuna mtu aliyeweka haya moyoni mwake.