\v 4 Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: "Yahwe asema hivi: Ona, nilichokijenga, sasa ninakirarua chini. Nilichopanda, sasa ninaking'oa. Nitafanya hivi kote duniani. \v 5 Lakini je, unategema mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja juu ya binadamu wote--hii ni tamko la Yahwe--lakini ninakupa maisha yako kama nyara popote utakakoenda."