\v 16 Kila mtu akulaye ataliwa, na adui zako wote wataenda utumwani. Kwa maana kila aliyekuteka nyara atatekwa, na nitawafanya wote wanaokuwinda kuwa mawindo. \v 17 Kwa maana nitaleta uponyaji juu yako; nitakuponya majeraha yako—hili ni tangazo la Yahwe—nitafanya hivyo kwa sababu walikuita: Mwenyekutupwa. Hakuna anayeujali Sayuni."