\v 19 Je! Umemkataa kabisa Yuda? Je, unaichukia Sayuni? Kwa nini umetupiga wakati hakuna uponyaji kwetu? Tulitumaini amani, lakini hapakuwa na kitu kizuri-na kwa wakati wa uponyaji, lakini tazama, kuna hofu tu. \v 20 Tunakubali, Bwana, makosa yetu, uovu wa babu zetu, kwa kuwa tumekukosea.