\c 31 \v 1 "Katika wakati huo—hili ni tangazo la Yahwe—Nitakuwa Mungu wa koo zote za Israel, na watakuwa watu wangu." \v 2 Yahwe anasema hivi, "Watu ambao wamenusurika na upanga wamepata kibali katika nyika; nitatoka nje kuwapa pumziko Israeli." \v 3 Yahwe alinitokea zamani na kusema, "Nimekupenda wewe, Israeli, kwa upendo wa milele. Kwa hiyo nimekuvuta kwangu kwa agano la uaminifu.