\v 12 Maana Yahwe asema hivi, "Tazama, wasiostahili ni lazima wanywe sehemu ya kikombe. Je mnadhani mtaachwa bila kuhadhibiwa? Hapana, maana hakika mtakunywa. \v 13 Maana nimekwisha apa kwangu mimi mwenyewe--asema Yahwe--Hiyo Bozra itakuwa hofu, aibu, magofu, na kitu cha laana. Miji yake yote itakuwa magofu daima.