sw_hab_text_reg/02/15.txt

1 line
324 B
Plaintext

\v 15 'Ole wake yule anayelazimisha majirani wake kulewa _unaonyesha hasira yako na kuwafanya walewe ili uweze kutazama uchi wao.' \v 16 Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako!Kunywa, na utafichua govi lako ambalo halijatahiriwa! Kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.