sw_gal_text_ulb/05/13.txt

1 line
351 B
Plaintext

\v 13 Mungu amewaiteni ninyi, ndugu, kwenye uhuru. Ila msiutumie uhuru wenu kama fursa kwa mwili. Badala yake kwa upendo mhudumiane ninyi kwa ninyi. \v 14 Kwa kuwa sheria yote imekamilika katika amri moja; nayo ni "Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe." \v 15 Lakini kama mkiumana na kulana, jiangalieni kwamba msijiharibu ninyi kwa ninyi.