sw_gal_text_ulb/03/06.txt

1 line
410 B
Plaintext

\v 6 Abraham "Alimwamini Mungu akahesabiwa kuwa mwenye haki". \v 7 Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu. \v 8 Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: "katika wewe mataifa yote yatabarikiwa". \v 9 Ili baadaye wale ambao wana imani wabarikiwe pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa na imani.