\v 24 Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano, kwa kuwa wanawake hawa wanafanana na maagano mawili. Mojawapo kutoka katika mlima Sinai. Huzaa watoto ambao ni watumwa. huyu ni Hajiri. \v 25 Sasa Hajiri ni mlima Sinai ulioko Arabuni. Hufananishwa na Yerusalem ya sasa, kwa kuwa ni mtumwa pamoja na watoto wake.