sw_ezr_text_reg/10/01.txt

1 line
401 B
Plaintext

\v 1 Wakati Ezra akiomba na kutubu, akalia na kujirusha chini mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa la wanaume Israel, wanawake na watoto wakakusanyika kwake, kwa kuwa watu walikuwa wakilia sana. \v 2 Shekania mtoto wa Yehieli, mwana wa Elamu akamwambia Ezra, "Tumekuwa sio waaminifu kwa Mungu na tumeoa wanawake wa kigeni kutoka nchi nyingine. Lakini pamoja na hilo, bado kuna tumaini kwa Israel.