sw_exo_text_reg/37/14.txt

1 line
371 B
Plaintext

\v 14 Pete hizo zilikuwa karibu na ule mzingo, ili kutegemeza ile miti ya kuibeba meza hiyo. \v 15 Halafu akafanya ile miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu ili kuibeba ile meza. \v 16 Baada ya hilo akafanya kutokana na dhahabu safi vile vyombo vilivyo juu ya meza, sahani zake na vikombe vyake na mabakuli yake na mitungi yake iliyotumiwa kumimina matoleo ya kinywaji.