sw_exo_text_reg/37/07.txt

1 line
454 B
Plaintext

\v 7 Bezaleli akafanya makerubi wawili wa dhahabu. Kwa kazi ya kufua akawafanya kwenye miisho yote miwili ya kifuniko. \v 8 Kerubi mmoja kwenye mwisho ule, na yule kerubi mwingine kwenye mwisho huu. Aliwafanya makerubi juu ya kifuniko kwenye miisho yote miwili. \v 9 Nao wakawa makerubi wanaonyoosha mabawa yao mawili kuelekea juu, wakisitiri kifuniko kwa mabawa yao, nazo nyuso zao zilikuwa zikielekeana. Nyuso za makerubi hao zilielekea kifuniko hicho.