sw_exo_text_reg/14/15.txt

1 line
581 B
Plaintext

\v 15 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Kwanini wewe, Musa, unaendelea kuniita mimi? Waambie Waisraeli waendelee mbele. \v 16 Nyanyua gongo lako juu, nyoosha mkono wako kuelekea baharini na uigawanye sehemu mbili, ili watu wa Israeli wapite baharini kwenye nchi kavu. \v 17 Jitahadharishe kuwa nitafanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu ili wawafuate. Nitapata utukufu kwasababu ya Farao na jeshi lake lote, magari yake ya farasi, na wapanda farasi. \v 18 Kisha Wamisri watajua kuwa mimi ni Yahweh nitakapo pata utukufu kwa sababu ya Farao, magari yake na farasi, na wapanda farasi wake."