sw_exo_text_reg/14/04.txt

1 line
399 B
Plaintext

\v 4 Nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, na yeye atawakimbiza. Nitapata utukufu kwa sababu ya Farao na jeshi lake lote. Wamisri watajua mimi ni Yahweh." Kisha Waisraeli wakaweka kambi kama walivyo elekezwa. \v 5 Mfalme wa Misri alipo ambiwa Waisraeli wametoroka, nia ya Farao na watumishi wake ikageuka dhidi ya watu. Wakasema, "Tumefanya nini kwa kuwaacha Waisraeli waende uhuru na wasitutumikie?"